Watu Shule is rated 3 out of 5 in the category e-learning. Read and write reviews about Watu Shule. Sisi ni timu ya watu wanaomini msemo wa "Elimu haikuanzia darasani, mama alianza kufundisha. Elimu haishii darasani, mtaa unaendelea kufundisha."- Rogers Katuma Watu wengi wamekosa fursa ya kuendelea kielimu kupitia mfumo wa kawaida wa elimu, kwenda shule, kufaulu na kupata cheti. Na watu wengi zaidi wanakosa fursa ya kujiendeleza kielimu baada ya sehemu waliyoishia shuleni kutokana na gharama, majukumu, muda na mfumo. Kiuhalisia mtaani kuna elimu, ujuzi na uwezo tofauti unaohitajika ili ufanikiwe hata kama hamna anayetoa cheti. Njia bora zaidi ya kujifunza ni kupitia ujuzi, elimu na uzoefu ambao umefanya kazi mtaani na kufikisha malengo ya watu. Na watu bora zaidi wa kufundisha ni wale ambao ujuzi, elimu na uzoefu wao mtaani umewafanya wafanikiwe. Sisi ni timu ya watu tunaotengeneza mazingira ya watu wenye ujuzi, elimu na uzoefu waliofanikiwa mtaani na kuifikisha kwa watu walioukuwa darasani na waliotoka darasani wakiwa kwenye safari yao ya mafanikio mtaani. Ndoto yetu ni kuhakikisha kila mwenye macho, masikio na simu apate ujuzi, elimu na uzoefu inayohitajika kufanikiwa mtaani. "Elimu haikuanzia darasani, mama alianza kufundisha. Elimu haishii darasani, mtaa unaendelea kufundisha."- Rogers Katuma
Address
7th Floor, Seedspace Tanzanite Tower, Victoria
Company size
51-200 employees
Headquarters
Dar es Salaam, Kinondoni